Thursday 27 November 2008

MAPENZI YA WEMA SEPETU NA KANUMBA YAZIDI KUNOGA

Masupastaa hao ambao wamekuwa katika uhusiano wa kimapenzi wa chinichini kwa muda mrefu, siku hiyo waliamua kudhihirisha penzi lao ambapo Wema alionekana kuwa hoi kwa Kanumba huku kila wakati akimshikashika mabegani.Hata hivyo, baada ya wapenzi hao kuona mambo sio mambo ndani ya ukumbi huo, waliamua kukokotana kuelekea kwenye gari yao kisha kutokomea gizani.Akizungumzia uhusiano wao Wema alisema kwamba, hasikii wala haambiwi kwa Kanumba kwani mapenzi anayopata hawezi kuyapata kwa mwanaume mwingine.Alisema kuwa, hata Kanumba mwenyewe kwake amefika na anaamini kwamba kweli anampenda kwani imefikia hatua ya kumuwekea mabaunsa wamlinde ili asije akaibiwa mali zake.‘’Jamani mapenzi ninayopewa na Kanumba hayasimuliki mimi mwenyewe nimesalimu amri na ningekuwa na uwezo ningewaonyesha walimwengu luningani. Kimsingi kwa Kanumba nimefika na yeye pia amefika maana hadi kuniwekea baunsa anichunge si mchezo, anapata vitu adimu,’’alijigamba Wema.Alipoulizwa juu ya tetesi kuwa Kanumba ameshapeleka posa kwa wazazi wake na kwamba anataka kumchukua jumla jumla Wema alikanusha uvumi huo na kudai kwamba, muda bado ila itafika wakati wa kufanya hivyo.

No comments: