Thursday, 19 March 2009

TID AMVISHA PETE YA UCHUMBA ANGERIS


Baada ya kujaribu kuficha sana kumweka hadharani mchumba wake aliyemvalisha pete wiki mbili zilizopita, hatimaye mchumba wa Khaleed Mohamed a.k.a TID amejulikana.
Chanzo chetu kimoja kimevumbua kuwa mchumba huyo si mwingine bali ni mwanamuziki wa Bongo Fleva anayekuja kwa kasi
Angeris Faber a.k.a Angie.
Inasemakana Angie amekuwa akishinda nyumbani kwa TID mitaa ya kinondoni na pia ndiye aliyevalishwa pete siku hiyo, katika mahojiano na waandishi wa habari siku moja Angie aliwahi kusema kuwa angehusudu siku moja kuwa karibu na TID.
Angie ni mmoja wa wanamuziki wenye kipaji waliovumbuliwa na lile shindano la Bongo Star Search mwaka jana, mpaka sasa ameshatoa nyimbo mbili zinazotamba kwenye vituo vingi vya Radio na Televisheni, wimbo wa “Mimi na Wewe” na “My Boo”.

No comments: