Saturday, 8 August 2009

MIRIAM GERALD ATWAA VODACOM MISS LAKE ZONE

Hatimae Miriam Gerald mrembo kutoka mkoa mwanza anyakua taji la vodacom miss lake zone,kulia kwake ni mrembo Mary Charles Alieshika nafasi ya pili, huku nafasi ya tatu ikirudi hukohuko mara kwa mrembo Sabina Budodi,namba nne ikishikiliwa na Glory Inosent mrembo kutoka Shinyanga,na namba tano alichukua mrembo Emakulata Alphonce kutoka Kagera,Mgeni rasmi katika shughuli hii alikuwa Mheshimiwa Naibu Waziri wa ushirikiano Afrika mashariki,MOHAMED ABOUD.Ambae aliwakabidhi washindi zawadi zao,namba moja alipewa hela ya kitanzania sh,laki sita,huku aliechukua nafasi ya pili akiondoka na sh,laki nne, na mshindi wa tatu sh, laki tatu, namba nne na tano walipewa sh laki moja na nusu.warembo wote walipewa zawadi zao ispokuwa mrembo namba tano Emakulata Alphonce kutoka kagera alipatwa na mshtuko na kupoteza faham aliposomwa na jaji mkuu kwamba ameshika namba tano,hivyo hakuweza kufika mbele kwani alikuwa amepelekwa hosipitali ya rufaa bugando,tunamshukuru mungu kwani sasa anaendelea vizuri.

1 comment:

Anonymous said...

kweli miriam ni haki yako kuwa miss lake zone. nakuombea uchukue taji la miss tanzania