Tuesday, 31 March 2009

HONGERA BW. NA BI. KIKWETE

Maisha ya ndoa ni safari ndefu.Wengi waliomo ndani ya ndoa wanakiri kwamba ni safari ndefu,ngumu inayohitaji uvumilivu na umakini wa hali ya juu lakini pia yaweza kuwa safari yenye kila aina ya raha na mafanikio.
Ndio maana unapotimiza mwaka au miaka fulani katika ndoa,ni jambo la kheri na linalostahili kusheherekewa.Hivyo ndivyo ilivyokuwa hapo jana wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Salma waliposheherekea miaka 20 ya ndoa yao.

Sherehe hiyo fupi ilifanyikia Ikulu jijini Dar-es-salaam na kuhudhuriwa na ndugu,jamaa na marafiki wa karibu wa “First Family” ya Tanzania.Pichani(juu) ni Rais Kikwete akimlisha keki mkewe Salma kusheherekea kumbukumbu hiyo.
Tunaungana na wote wanaowatakia kheri kuwapongeza na kuwatakia kila la kheri katika maisha yao.

No comments: